About the Show

Utengenezaji wa Don’t Lose the Plot

Nini kinatokea pale wakulima wachanga wanne, kijana mmoja na binti mmoja kila mmoja kutoka Kenya na Tanzania, wote wanapewa ekari moja ya shamba kulima sako kwa bako katika msimu wote wa kilimo kwa nafasi ya kushinda kipande cha ardhi?

Kipindi cha televisheni cha kusisimua kama vile haujawahi kuona tena!

_DSC5856.jpgDon’t Lose the Plot (DLTP) Ni mkondo mpya katika kipindi cha ukulima. Kinaleta muundo flani wa televisheni yakinifu -  Uboreshaji na shindano – kwa rahisi na mpya , yenye kuhamasisha vijana wa Kenya na Tanzania katika ukulima kama biashara na, kama njia ya kuboresha maisha yao.

Washiriki watakua wakishindana moja kwa moja – kila mmoja akingangana kuwa mkulima mwenye faida na mawazo ya kibiashara na shupafu katika kundi.

Nani atakua mshindi wetu mwishoni? Fatilia kila wiki wakati maarifa na ujanja inapoendelea kushamiri.

_DSC5917.jpg

Sisi ni Nani

Sisi ni kundi la wataalamu tuliyojitolea kuboresha maendeleo endelevu na uboreshaji wa maisha ya watazamaji wengi ndani ya Afrika, kipindi kimoja cha tevelisheni kwa wakati.

Don’t Lose the Plot ni kipindi cha nne kutayarishwa na The Mediae Company vipindi vingine vikiwa Shamba Shape Up, Makutano Junction na Know Zone. Mediae huendeleza elimu, burudani na ufanisi wa vyombo vya habari, wakisambaza maarifa muhimu na taarifa kwa njia ambazo zinaweza kufikia wengi na kueleweka.

_DSC5435.jpg

_DSC5473.jpg

Lengo letu

Kuchafua mikono shambani haiwapendezi sana vijana. Kwa wastan umri wa wakulima wa Afrika ni miaka 60, ni wakati sasa kilimo kipate sura mpya.

Tunataka kukuza ukulima kati ya vijana kama chakujivunia na taaluma yenye manufaa,ili kuhakikisha maisha ya baadae yenye uhakika wa chakula.

_DSC5235.jpg

Kipindi kinalenga kupunguza tikadi na vizuizi vya kijamii na aibu za kihisia vya kuanzisha biashara ndogo, kukabiliana na machukizo ya kijamii dhidi ya kilimo na shughughuli zake, na kuwaami vijana wenye nia na uwezo wa jasiriamali kwa elimu ya msingi kwa mchakato wote wa uzalishaji hadi mauzo . Hii vile vile itaelimisha vijana katika njia na nafasi mbali mbali zilizopo ili kuingia na kukuza vitendo vya kiuchumi vya kilimo.

Don’t lose the Plot ni njia ya kutoa motisha ili kuongeza uzalishaji wa kilimo zaidi ya mahitaji tu yakinyumbani, kusimamisha vijana kuhamia mjini toka mashambani, na ku bandilisha dhana potovu kuhusu kilimo.

Kimsingi, kujifunza kutoka kwa washiriki na kuiga, watazamaji kwa hakika watapata msukumo, kumiliki, kukodi na kuendesha mashamba na biashara za kilimo