Maboga

Maboga au matango yana soko zuri. Pia ni mazuri kwaajili ya kuliwa na wewe na familia yako kwani yana vitamin vingi.

Yanakua vyema kwenye maeneo ya mwinuko wa mita 1700 kutoka usawa wa bahari na nyuzi joto 23-29°C.. Hayafanyi vyema kwenye maeneo yenye baridi.

Kama ungependa kupanda maboga, hakikisha udongo wako hautoti maji kama vile udongo laini au mchangarawe na unakiwango cha uchachu au pH ya 6.0-6.5.

Kujua kiwango cha uchachu au pH cha udongo wako au kiasi cha asidi ,utahitaji kufanya kipimo cha udongo. Kipimo cha udongo ni muhimu kwasababu kitakujulisha:

  • Udongo wako una afya kiasi gani
  • Mbolea gani ya kuongeza kufanya udongo wako kuwa bora.
  • Zao gani litakua vizuri kwenye udongo wako.

Acha udongo wako upimwe na Daktari Wa Udongo kutoka CropNuts. Wapigie kwenye +254 790 499190 au tuma barua pepe kwa support@cropnuts.com. Watachukua sampuli ya udongo wako kutoka shambani kwako kwaajili ya kupima na watakutumia majibu. Kipimo cha udongo kinaokoa pesa na kitakupa mazao makubwa na bora.