Uandaaji wa shamba na Kupanda

Ploughing land preparation

Uandaaji wa shamba

Lima shamba lako mapema. Unahitaji kuchimba kina cha sentimita 20-30 kwenda chini kwenye udongo. Vunja madongo ya udongo.Changanya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Lainisha udongo wa juu. Kama shamba lako liko kwenye eneo la mvua nyingi, fanya matuta yaliyoinuka.


Kupanda

Panda mbegu sentimita 45 kiumbali kwenye mishororo ya sentimita 90 kiumbali. funika mbegu na angalau sentimita 2 ya udongo. 

Butternut spacingWakati wa  kupanda, ongeza DAP au NPK 17:17:17.Tumia kilo 80 kwa ekari.

Kujazia

Jazia kutumia CAN wakati vikonyo au vishina vina urefu wa kama sentimita 30. Tumia kijiko cha mezani/chakula 1-2 kwa mmea.Utahitaji takriban kilo 100 za CAN kwa ekari.

Magugu/kwekwe

  • Magugu/kwekwe huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mmea wako. Yanaweza kudhuru vibaya mmea wako katikati wakati mashina yanachomoza na wakati vikonyo vinakua.
  • Magugu/kwekwe pia yanaficha wadudu na magonjwa.
  • Anza kupalilia wakati mimea ya maboga ina wiki 2.Ng’oa magugu wakati unayaona.Vikonyo na majani ya maboga yanavyokua, utagundua una magugu kidogo.

Uchavushi

Butternut pollinationMaboga yana maua ya kike na ya kiume. Maua yanahitaji kuchavushwa kwaajili ya tunda kukua vyema. Hii inamaanisha kwamba nyuki wanatakiwa kutembelea ua la kiume, kisha ua la kike. Wavutie nyuki kwa viraka vya maua kwenye shamba lako. Unaweza pia kufuga nyuki na kuuza asali.

Jazia tena mwezi 1 baadae wakati yanaanza kutoa maua. Utahitaji takriban kilo 100 za CAN kwa ekari.