Uvunaji na Kuhifadhi

Butternut squash

Maboga yanatakiwa kuwa tayari kwa kuvunwa baada ya siku 75-150. Yanapaswa kukomaa kwenye mmea.Ukivuna mapema sana, hayatakua na kiwango kizuri. Ngozi inatakiwa iwe ngumu na isikwangurike/kwaruzike kiurahisi.

Vuna tunda likiwa na sehemu ya shina. Kuwa makini usiharibu tunda wakati wa kuvuna. Litahifadhika kwa muda mrefu.

Hifadhi maboga kwenye sehemu kavu na baridi mpaka bei sokoni iwe nzuri.Hifadhi mpaka miezi 4.