Kupanda Dhania
Baada ya uandaaji wa shamba mzuri:
Hatua ya 1
Fanya matuta 30cm kiumbali kwa uzalishaji wa majani machanga na 50cm kiumbali kwa uzalishaji wa mbegu.
Hatua ya 2
Changanya vyema samadi na mbolea ya kupandia kwenye matuta. Unahitaji ndoo 12 za samadi kwa kila mita 1 ya mraba ya shamba. Tumia mbolea ya kupandia kama Mavuno Vegetable fertilizer N.P.K 20.10.18 na baadae jazia na Mavuno Topdressing N.P.K 26.0.0.
Hatua ya 3
Panda mbegu 2-3 kuingia ndani na funika taratibu na udongo. Unahitaji kilo 2 za mbegu kwa ekari
Hatua ya 4
Mwagilia maji mara kwa mara kwa mfano mara 2-4 kwa wiki. Hii ni wakati udongo ni mkavu na epuka kukusanyika kwa maji. Upungufu wa maji pia utapelekea kupevuka haraka ( utengezaji wa mbegu mapema)
Hatua ya 5
Uchipukaji unaanza kati ya siku 7-10 baada ya kupanda
Hatua ya 6
Fanya ondoa mimie zaidi na acha yenye afya wakati wa mimea ina urefu wa sentimita 5-7 ili kuacha sentimita 10-15 katika mshororo.
Hatua ya 7
Unaweza kukata wakati ina urefu wa nusu futi ili kuhamasisha ukuaji wa zaidi
Hatua ya 8
Itachukua wiki 4-6 kwa majani ya kijani kukomaa na miezi 3-4 kwa mbegu
Inapendekezwa kupanda mbegu moja
kwa moja kwenye kitalu kilicho tayari. Kupandikiza kunasababisha utoaji maua
mapema. Nunua mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wauzaji wa kuaminika.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Dhania
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure