Uvunaji

Cooking coriander

Unaweza kupanda dhania kwaajili ya majani au mbegu.

Upandaji dhania kwaajili ya majani     

Majani ya dhania yanachukua mwezi 1 na nusu kukomaa. Ukipanda kwaajili ya majani, fanya ukataji kadhaa wakati wa kukua.

Uvunaji wa kwanza unatakiwa kufanywa wakati mimea ina kimo cha nusu futi (10-15cm)

Hii itasisimua ukuaji wa machipukizi zaidi. Unahitaji kufanya ukataji mara 4-5 wakati wa msimu wa kukua kwaajili ya mtishamba wa kijani. Hii itakupatia wastani wa mavuno ya tani 2.8- 4 kwa ekari.

Unaweza kukatakata majani na kupika na chakula.

Kupanda dhania kwaajili ya mbegu

Mbegu huchukua miezi 3-4 kukomaa. Wakati maua yamekauka, kata taraibu mashina na kausha kwenye turubai safi kwa siku 2-3. Mwishoni pepeta na uchunge kupata mbegu safi za dhania. Kama itahudumiwa vyema, unaweza kupata kilo 480-680 za mbegu kwa ekari. Daima vuna asubuhi mapema au jioni kupunguza upotevu kutokana na kuvunjika. Kisha kutengenezwa kupata viungo mchanganyiko na poda ya mchuzi.

Coriander seeds