Kupanda Dhania

Coriander leaves

Baada ya uandaaji wa shamba mzuri: 

Hatua ya 1

Fanya matuta 30cm kiumbali kwa uzalishaji wa majani machanga na 50cm kiumbali kwa uzalishaji wa mbegu.

Land preparationHatua ya 2

Changanya vyema samadi na mbolea ya kupandia kwenye matuta. Unahitaji ndoo 12 za samadi kwa kila mita 1 ya mraba ya shamba. Tumia mbolea ya kupandia kama Mavuno Vegetable fertilizer N.P.K 20.10.18 na baadae jazia na Mavuno Topdressing N.P.K 26.0.0.

Planting potatoes mix with manureHatua ya 3

Panda mbegu 2-3 kuingia ndani na funika taratibu na udongo. Unahitaji kilo 2 za mbegu kwa ekari

Sowing corianderHatua ya 4

Mwagilia maji mara kwa mara kwa mfano mara 2-4 kwa wiki. Hii ni wakati udongo ni mkavu na epuka kukusanyika kwa maji. Upungufu wa maji pia utapelekea kupevuka haraka ( utengezaji wa mbegu mapema)

Hatua ya 5

Uchipukaji unaanza kati ya siku 7-10 baada ya kupanda

Germination_corianderHatua ya 6

Fanya ondoa mimie zaidi na acha yenye afya wakati wa mimea ina urefu wa sentimita 5-7 ili kuacha sentimita 10-15 katika mshororo.

Coriander thinningHatua ya 7

Unaweza kukata wakati ina urefu wa nusu futi ili kuhamasisha ukuaji wa zaidi

Coriander cuttingHatua ya 8

Itachukua wiki 4-6 kwa majani ya kijani kukomaa na miezi 3-4 kwa mbegu

Coriander leaves 2Inapendekezwa kupanda mbegu moja kwa moja kwenye kitalu kilicho tayari. Kupandikiza kunasababisha utoaji maua mapema. Nunua mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wauzaji wa kuaminika.