Uandaaji wa shamba na Kupanda
Uandaaji wa shamba
Lima shamba lako mapema. Unahitaji kuchimba kina cha sentimita 20-30 kwenda chini kwenye udongo. Vunja madongo ya udongo.Changanya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Lainisha udongo wa juu. Kama shamba lako liko kwenye eneo la mvua nyingi, fanya matuta yaliyoinuka.
Kupanda
Panda mbegu sentimita 45 kiumbali kwenye mishororo ya sentimita 90 kiumbali. funika mbegu na angalau sentimita 2 ya udongo.
Wakati wa kupanda, ongeza DAP au NPK 17:17:17.Tumia
kilo 80 kwa ekari.
Kujazia
Jazia kutumia CAN wakati vikonyo au vishina vina urefu wa kama sentimita 30. Tumia kijiko cha mezani/chakula 1-2 kwa mmea.Utahitaji takriban kilo 100 za CAN kwa ekari.
Magugu/kwekwe
- Magugu/kwekwe huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mmea wako. Yanaweza kudhuru vibaya mmea wako katikati wakati mashina yanachomoza na wakati vikonyo vinakua.
- Magugu/kwekwe pia yanaficha wadudu na magonjwa.
- Anza kupalilia wakati mimea ya maboga ina wiki 2.Ng’oa magugu wakati unayaona.Vikonyo na majani ya maboga yanavyokua, utagundua una magugu kidogo.
Uchavushi
Maboga yana maua ya kike na ya kiume. Maua yanahitaji kuchavushwa
kwaajili ya tunda kukua vyema. Hii inamaanisha kwamba nyuki wanatakiwa
kutembelea ua la kiume, kisha ua la kike. Wavutie nyuki kwa viraka vya maua
kwenye shamba lako. Unaweza pia kufuga nyuki na kuuza asali.
Jazia tena mwezi 1 baadae wakati yanaanza kutoa maua. Utahitaji takriban kilo 100 za CAN kwa ekari.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Maboga
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure