Wadudu na Magonjwa

Cucumber beetle

Wadudu

Cucumber Beetle

Cucumber Beetles hula kwenye mashina, majani na matunda ya mmea wako wa maboga. Kawaida utawaona ndani ya maua. Wanataga mayai kwenye udongo. Kiluilui/Buu hula mizizi ya mmea ya maboga.

Waue Cucumber Beetles kwa Nimbecidine kutoka Osho Chemicals. Changanya 30ml za Nimbecidine na lita 20 za maji kwenye bomba/knapsack. Nyunyizia mimea siku 15 baada ya kupanda.Rudia kila siku 15-20

Melon flies na White flies

Melon flies hula kwenye mashina, majani, mizizi na tunda la mmea wako wa maboga.White flies hunyonya maji kutoka kwenye majani.

White flies pia hubeba virusi vya Cucumber Mosaic Virus(CMV). CMV hushambulia majani na kusababisha ukuaji duni na majani yaliojiunda vibaya.

Angamiza Melon Flies na White Flies kwa Asataf kutoka Osho Chemicals. Changanya gramu 20 za Asataf na lita 20 za maji kwenye Bomba/knapsack. Nyunyizia wakati ukiona melon flies au white flies.Nyunyizia tena baada ya siku 10 kama wameshambulia vibaya. Kama sivyo, nyunyizia baada ya siku 21.

Magonjwa

Powdery Mildew

Powdery mildew butternutKuvu la majivu jivu au Powdery Mildew ni kuvu wanaovamia majani.Tibu Powdery Mildew kwa Control kutoka Osho Chemicals.

Changanya gramu 12 ( kijiko cha chakula/mezani) cha Control na lita 20 za maji kwenye snapsack. Nyunyizia maboga yako kila siku 14.