Pilipili Hoho

Inajulikana sana kama Pilipili hoho hapa Kenya, Hoho ni aina ya mmea imara ambao ni nadra sana kushambuliwa na magonjwa na wadudu, japo unahitaji kinga nzuri kwa uangalifu.

Hoho inakua vyema katika hali ya hewa ya 2,000M na mvua ya kiwango cha kati takriban 600 -1200mm kwa mwaka. Hali ya joto kwaajili ya ukuaji ni 15ºC-25 ºC.

Pia zinaota vyema kwenye udongo ulio na uchachu/asidi au pH ya 6.0 -6.5.

Hapa Kenya,ukulima wa hoho unafanya vyema katika maeneo yenye joto kama vile Mkoa wa Mashariki na Ukanda wa Pwani.