Kupandikiza miche ya Hoho

Plantraisers Capsicum seedlings

Panda hoho katika kivungulio. Utapata mavuno mengi na bora na kutakua na wadudu wacheche. Chagua aina nzuri kutoka Royal Seed. Nunua miche badala ya mbegu kwasababu:

  • Utapata mmea haraka – miche inakuokolea mwezi mmoja.
  • Hautapoteza miche mingi kwa wadudu na magonjwa
  • Hauhitaji kitalu kwani miche inaweza kupandwa hapo kwa hapo

Plant Raisers wanapanda miche kwenye treya na udongo safi ili kuzuia wadudu na magonjwa.

Hauhitaji kuongeza mbolea wakati wa kupanda.

Hatua ya 1

Tumia umwagiliaji wa tone kwa tone ili mimea yako ipate maji ya kutosha na mbolea. Kila mmea unahitaji ½ lita ya maji kila siku.

Capsicum planting dimensions

  • Chora zigizaga kwenye kitalu kati kati ya mipira ya maji.
  • Panda miche karibu na mashimo katika mipira ya maji. Maji zaidi yataingia kwenye mizizi na kidogo yatapotea. Mashimo ya dripu lazima yaangalie upande wa juu.
  • Panda miche sentimita 60 kiumbali. Kama ikiwa karibu sana wakati ikiwa mikubwa haitakua vyema.

Hatua ya 2

Angalia unyevu wa udongo kwa kutumia mkono wako. Kukagua kama mimea yako inapata maji wa kutosha , chota udongo ujazo wa kuganja.

Checking soil moisture

  • Kama udongo umetota sana, utakwama kwenye mikono yako na kuwa kama mpira utakapoifinya. Ya ziada, kama mmea una meji mengi sana utaanguka na shina kuoza. Hii inaitwa kudodosha( Dymping off) na mmea unaweza kufa.
  • Kama udongo ni mkavu sana, hautaganda kabisa.

Hatua ya 3

Katika wiki 2 za mwanzo, mwagilia miche maji mara 2-3 kwa wiki. Baada ya wiki 2, mwagilia maji kila siku. Hii inafanya mizizi izame ndani kwenye udongo na kuifanya imara. Mimea itaota vyema na kukupa mazao mazuri.

Usimwagilie maji mimea yako wakati wa jioni. Udongo utatota sana usiku kucha na utapata magonjwa zaidi.