Uhudumiaji wa mmea

Capsicum crop management

Kwaajili ya mavuno mazuri ya Hoho, unataka utoaji sawasawa wa matunda kwenye mmea.

Virutubisho vingi vinatoka kwenye udongo. Kama kuna matunda mengi sehemu ya chini, yatatumia virutubisho vyote. Virutubisho havitasafiri kufikia matunda ya juu na yatakufa.

Kagua unyevu wa udongo

Tumia mikono yako kukagua udongo umetoete kwa kiasi gani kila siku. Kama udongo ni mkavu, mmea haiwezi kupata maji na virutubisho. Utapata mavuno mabaya. Usimwagilie maji mimea yako wakati wa jioni. Udongo utatota sana usiku kucha na utapata magonjwa zaidi.

Checking soil moistureKutegemeza hoho zako

Matunda ya hoho ni mazito. Tegemeza/usitiri mmea wako wa Hoho kwa waya.

Supporting capsicumFunga mmea kwenye waya kwa kutumia uzi. Zungusha mmea kuzunguka uzi. Kua mwangalifu usiumize mmea. Kutegemeza Hoho zako kunasidia mzunguko wa hewa. Utakua na wadudu wachache na magonjwa.

Pogoa mmea wako wa Hoho kila wiki

Kupogoa kunaruhusu mmea wako kutumia maji na virutubisho kutengeneza matunda makubwa, yote yakiwa na ukubwa sawa.Toa matunda madogo na yoyote yenye umbo mbaya.

Hatua ya 1

Toa vikonyo vya pembeni. Acha vikonyo 2 kwa kila mmea. Toa majani yaliyozeeka na majani yenye magonjwa. Mmea wako utakua na afya.

Pruning_remove side shootsHatua ya 2

Toa matunda ya mwanzo, ili mmea ukue vyema. Toa matunda ya ziada ili yele yanayoachwa yawe makubwa.

Pruning_remove first fruitSafisha kivungulio chako mara kwa mara

Palilia kila wiki kutumia mkono.Nyasi huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mmea wako.

Kwekwe/Magugu/nyasi pia huficha wadudu na magonjwa. Kagua wadudu na magonjwa kila siku.

Unaweza pia kuzuia kwekwe kwa kutumia nyasi kavu kufunikia.

Capsicum weeding