Benki na Ukulima

Banking and Farming

Benki inaweza kukusaidia kuendesha shamba lako kama biashara, kuwa na msaada wa kifedha kunaweza kwa mara nyingi inaweza  kukusaidia kufikia malengo yako au kwa haraka zaidi.

Kuna sababu nyingi nzuri kwanini kuwa na akaunti ya benki ni wazo zuri:

  1. Inakuzuia kuwa na fedha nyingi nyumbani, ambazo zinaweza kuibiwa.
  2. Inakusaidia kuweka akiba kufikia malengo yako na kuweka akiba.
  3. Inakusaidia kupanga kwaajili ya baadaye.

Kufungua akaunti ni rahisi. Unahitaji tu kuwa na kitambulisho cha kitaifa na kujaza fomu. Hata watu wenye tatizo la kusoma wanaweza kufungua akaunti ya benki kwani watu wa benki wanaweza kukusaidia kujaza fomu.

Hata hauhitaji pesa yoyote ya kuanzia ili kufungua akaunti ya benki, unaweza obgeza pesa unavyoendelea!

Unaweza pia kupata mkopo kutoka benki unapokua na akaunti kama unataka kufanya shamba lako kuwa biashara kubwa.

Farming and bankingUnaweza kupata mkopo kwaajili ya ng’ombe, kuku, ujenzi au mbegu.

Mikopo inaweza kuwa njia nzuri ya kuanza au kupanua biashara yako. Ni muhimu sana muda wote kulipa mikopo yako. Inakupa kiwango kizuri cha muamana na historia ya mkopo.Unapoomba mkopo, benki itataka kujua historia yako ya madeni. Wanaweza kuangalia:

  • Idadi ya deni/mkopo kwenye akaunti yako ya MPESA. Unaweza kuchapisha historia yako ya MPESA
  • Kama umelipa mikopo yako ya awali kwa muda muafaka
  • Muda wako wa maongezi.
  • Malipo kama vile ada ya shule, stima na bima – unalipa kwa muda muafaka?

Kama una historia nzuri ya madeni, benki inaweza kukupa mkopo

Benki hupitisha mkopo ndani ya siku 2, na kawaida utalipa mkopo kwa miezi 18.

Kama una akaunti ya benki, benki inaweza kukusaidia kutengeneza mpangilio wa biashara ili uweze kutengeneza pesa zaidi.

Kwa taarifa zaidi kuhusu benki, wasiliana na huduma yetu ya taarifa kwenya iShamba.