Kugharamia kifedha biashara yako

Je mikopo ni mibaya?

Mikopo inaweza kuwa mizuri au mibaya kutegemea na sababu kwanini mkopo ulichukuliwa. Kama unachukua mkopo ambao utatumia kuwekeza kwenye mradi ambao itakupatia pesa na ambao itakua kithamani, basi hicho kinachukuliwa ni mkopo mzuri. Kwa mfano, kutumia mkopo kuwekeza kwenye shamba lako kuzalisha kipato zaidi kwako na kwa familia yako kwani utakua na mavuno mengi na bidhaa ya kiwango bora. Hivyo, usiogope kuchukua mkopo kwaajili hii. Hata hivyo, mkopo ya kibinafsi mara nyingi huonekana kana mkopo mbaya kwani hauzalishi pesa, na utahitajika kulipa mkopo.