Kusimamia biashara yako
![Budgeting](/media/images/DLTP_contestants_budgeting.min-200x200.png)
Kufanikiwa katika kila tendo shambani mwako:
- Weka kumbukumbu nzuri zikusaidie kusimamia vyema.
- Jiunge na kikundi cha wakulima ili kufanya kazi na wakulima wengine kwaajili ya maarifa bora na bei nzuri.
- Tambua biashara yenye kutoa pesa nyingi zaidi. Kwa mfano, kama watengezaji wa kachiri na chips/vibanzi wananunua kwa bei nzuri, unahitaji kupanda viazi.
- Pata cheti cha KEBS ili kuuzia maduka makubwa na wanunuzi wakubwa
- Mkataba wa kupanda: tafuta mnunuzi kabla ya upandaji na upange kwaajili yao kununua mazao yako unapovuna.
- Jua kiasi gani wanunuzi wanataka kununua. Hii itakuambia bei za kuweka.
- Wekeza faida yako tena kwenye biashara.
- Kutoka kwenye faida unayopata, anzisha biashara nyingine, kama vile ufugaji wa kuku. Hii inakupa usalama kama moja kati ya biashara zako ina matatizo au isipofaulu.