Huduma ya pesa kutumia simu ya mkononi

MPESA

Kutumia simu yako unaweza kuhifadhi pesa, kupata mkopo au kupata bima. Mara nyingi hautalazimika kwenda benki – unaweza kufanya hili ukiwa nyumbani kwako.

Kuhifadhi pesa, kutuma pesa kutoka MPESA/ akaunti ya pesa ya simu ya mkononi kwenda kwenye akaunti ya kuhifadhi pesa. Akaunti nyingine zinalipa riba.Hii inamaanisha benki inakulipa kiasi kidogo cha fedha ili kuweka pesa kwenye akaunti.Ken using mobile moneyWekea bima mazao yako kupitia simu yako

Tumia simu yako kupata bima kwaajili ya mazao yako.Angalia pakiti za mbegu zinazokuja na bima. Zina cheti/vocha zinazokueleza jinsi ya kupata bima ya mazao yako. Fuata maelezo yaliyopo kwenye vocha.

No rainOngea na kampuni ya bima ili kuelewa vyema jinsi inavyofanya kazi. Kama hakuna mvua na mbegu zako zisiote, itabidi ufanye madai kurudisha pesa zako. Kama kuna mvua, utapata mavuno!

KUMBUKA: Inabidi ulipie kwa kila utoaji unaofanya kutoka kwenye simu yako. Angalia gharama ya huduna yoyote ya simu kabla ya kujaribu.