Huduma ya pesa kutumia simu ya mkononi

Kutumia simu yako unaweza kuhifadhi pesa, kupata mkopo au kupata bima. Mara nyingi hautalazimika kwenda benki – unaweza kufanya hili ukiwa nyumbani kwako.
Kuhifadhi pesa, kutuma pesa kutoka MPESA/ akaunti ya pesa ya simu ya
mkononi kwenda kwenye akaunti ya kuhifadhi pesa. Akaunti nyingine zinalipa
riba.Hii inamaanisha benki inakulipa kiasi kidogo cha fedha ili kuweka pesa
kwenye akaunti.
Wekea bima mazao yako kupitia simu yako
Tumia simu yako kupata bima kwaajili ya mazao yako.Angalia pakiti za
mbegu zinazokuja na bima. Zina cheti/vocha zinazokueleza jinsi ya kupata bima
ya mazao yako. Fuata maelezo yaliyopo kwenye vocha.
Ongea na kampuni ya bima ili kuelewa vyema jinsi inavyofanya kazi. Kama
hakuna mvua na mbegu zako zisiote, itabidi ufanye madai kurudisha pesa zako.
Kama kuna mvua, utapata mavuno!
KUMBUKA: Inabidi ulipie kwa kila utoaji unaofanya kutoka kwenye simu
yako. Angalia gharama ya huduna yoyote ya simu kabla ya kujaribu.