Jinsi ya kuandaa mpango wa Biashara

Business plan

Biashara zote nzuri zinahitaji mpangilio. Panga vyema na utatengeneza pesa zaidi. Mpangilio wa biashara unakufanya uangazie malengo yako makuu. Unakutaarifu ulikotoka, umefikia wapi kwa sasa, na ni wapi unahitaji kuenda kama biashara.

Inaweza pia kukusaidia kupata mkopo kutoka benki, inasaidia watu kukukopesha pesa na inawaeleza watu unataka biashara yako iwe vipi katika muda wa miaka 3 mpaka 5.



Hatua ya 1: Muhtasari na maelezo ya biashara

Moja ya vitu vya kwanza unachohitaji kufanya ni kuandika muhtasari wa biashara na maelezo. Hii itakusaidia wewe na wengine kuelewa nini unachotarajia kufanikisha:

  • Muhtasari wa Biashara: Nini unataka kufanya? Wapi? Vipi? Kwa kiasi gani?
  • Maelezo ya Biashara: Nini kinatokea leo? Nini kinaweza kutokea hapo mbeleni katika eneo lako? Unaweza kufanya nini? Unaweza kuifanya vipi? Kitatengeneza vipi pesa?

Hatua ya 2: Mpango wa uzalishaji

Production planHakikisha muda wote una kitu cha kuuza kwa mfano ng’ombe wa maziwa. Kama ng’ombe wako wote watazaa kwa wakati moja, hautakua na maziwa ya kuuza. Kama una ng’ombe mmoja anaetoa maziwa, nini kitatokea kama akiwa mgonjwa?

Mara nyingine ni vizuri kuwa na biashara zaidi ya moja. Jaribu kufuga kuku au kupanda mboga.

Hatua ya 3: Mpango wa Masoko

Marketing planAngalia soko. Nini kinatokea katika soko kwaajili ya biashara yako leo? Hatua muhimu ni kutambua mnunuzi kwaajili ya zao lako, kuhakikisha unahudumia kuendana na mahitaji. Hii itahakikisha unapata rejesho katika uwekezaji wako.

Kuna Ushindani gani hapo? Kama una mshindani, unahitaji kufikiria jinsi unavyoweza kuwa tofauti na kutoa thamani nzuri kwa wateja wako. Utafanya nini kama mshindani akitokea?

Zingatia P 4 zifuatazo – Bei, Bidhaa, Ukuzaji na Mahali:

  • Uza kwa bei nzuri. Tambua kiasi majirani zako wanachouzia maziwa. Kama bei iko juu sana watu hawatanunua maziwa yako.
  • Bidhaa yako ni gani? Katika hili je maziwa ni safi na mabichi( Haijakaa).
  • Watu wanajuaje kama unauza maziwa? Unahitaji kutangaza . Bango/ Tangazo mlangoni? Kuwajulisha watu kanisani?
  • Wapi watu wanaweza kununua maziwa yako? Nyumbani kwako? Unapeleka? Kwenye OLX au mtandao wa kijamii?

Kwa taarifa zaidi kuhusu kujua masoko bonyeza hapa.

Hatua ya 4: Mpango wa kifedha

Financial planUzalishaji na utafutaji masoko unagharimu pesa. Unahitaji kiasi gani cha fedha? Je utahitaji mkopo? Una akiba ambazo unaweza kutumia?

Utahitaji kuandaa bajeti. Panga bajeti yako kukopa, kuweka akiba, kuwa na pesa za kuendesha na kukuza biashara yako, na kiasi gani unaweza kujilipa.

Hatua ya 5: Mpango wa kuendesha biashara

Jinsi gani biashara itaendeshwa siku baada ya siku? Je utahitaji watu wa kukusaidia? Je utahitaji kufanyia ukarabati vifaa vyako na je unahitaji usafiri?

Hatua ya 6: Mkadirio ya hatari

Matatizo inaweza kutokea wapi? Ni muhimu kuwaza kwa kina kuhusu hatari , kwa mfano; Utafanya nini kama mavuno ya mazao yako ni mabaya na kama ng’ombe wako akiwa mgonjwa.