Kusimamia biashara yako

Budgeting

Kufanikiwa katika kila tendo shambani mwako:

  • Weka kumbukumbu nzuri zikusaidie kusimamia vyema.
  • Jiunge na kikundi cha wakulima ili kufanya kazi na wakulima wengine kwaajili ya maarifa bora na bei nzuri.
  • Tambua biashara yenye kutoa pesa nyingi zaidi. Kwa mfano, kama watengezaji wa kachiri na chips/vibanzi wananunua kwa bei nzuri, unahitaji kupanda viazi.
  • Pata cheti cha KEBS ili kuuzia maduka makubwa na wanunuzi wakubwa
  • Mkataba wa kupanda: tafuta mnunuzi kabla ya upandaji na upange kwaajili yao kununua mazao yako unapovuna.
  • Jua kiasi gani wanunuzi wanataka kununua. Hii itakuambia bei za kuweka.
  • Wekeza faida yako tena kwenye biashara.
  • Kutoka kwenye faida unayopata, anzisha biashara nyingine, kama vile ufugaji wa kuku. Hii inakupa usalama kama moja kati ya biashara zako ina matatizo au isipofaulu.

Diversifying business