Ukulima na upatikanaji wa Soko
Masoko ni muhimu kwasababu yanasaidia wakulima kuuza na kupata pesa kwaajili ya biashara zao.
Kama mkulima, lazima upeleleze jinsi utakavyouza mazao yako kabla ya kuanza kupanda au kuotesha kitu chochote.
Kuna vitu 4 muhimu vya kuzingatia wakati unatafuta masoko.
Bidhaa
Hiki ni kile unachoamua kuuza baada ya kuchunguza mienendo ya soko. Wakati unapanga bidhaa gani unataka kuzalisha, fikiria kuhusu yafuatayo:
- Wengine wanazalisha nini?
- Je kuna uhitaji wa bidhaa yako?
- Soko linahitaji nini? Matarajio gani ya ubora yako katika eneo la soko?
- Mahitaji gani ya kisheria unatakiwa kutimiza? Kwa mfano, huwezi kuzungusha maziwa bila ya kibali.
Ni muhimu kwako kupanga
uzalishaji, tathmini kiwango cha uwekezaji kinachohitajika kwatika msimu wote,
jenga mazao/ ufugaji wa mfugo muhimu, gundua pembejeo zinazohitajika na ujue
makadirio ya kipato utakachopata ili uwe na ufanisi na biashara yenye
mafanikio.
Bei
Unahitaji kutafakari ni jua utakayotoza.
- Utatoza bei sawa na wengine?
- Utafanya nini kama kutatokea mshindani?
- Je inafidia gharama zako za uzalishaji na kukuachia faida?
- Kuna bei tofauti kulingana na viwango tofauti?
- Unawza kutengeneza faida? Kumbuka, unaweza kupata faida kama unauza vingi kwa bei nafuu kuliko kuuza kidogo kwa bei ya juu.
Unahitaji kujifunza matarajio ya kiwango katika soko kupunguza ukataliwaji wa bidhaa au malipo ya bei sawa sawa na gharama inayohusishwa na uuzaji na vitendo vyote husika katika kufikisha bidhaa sokoni.
Unatakiwa pia kuhakikisha kwamba unajua bei inayoendana na soko kwa ujumla. Haya yanapatikana kama ukijisajili na iShamba kwa kutuma ujumbe wa neno VIJANA kwenda 21606.
Mahali
Unahitaji kupanga kuhusu wapi utauza bidhaa yako sawa sawa na jinsi utakavyofikisha bidhaa yako kwa wateja wako.
Kuna njia 2 kuu kwa wakulima kama
wewe mwenyewe kuuza bidhaa zako:
Masoko yasiyo rasmi
Hizi ni njia rahisi sana za kufikia masoko. Zinajumuisha kuuzia hapo mlangoni mwa shamba na uuzaji wa kando ya barabara, masoko ya vijijini, vituo vya uratibu vya vijijini na uuzaji katika maeneo ya mjini, masoko ya jumla na rejareja kwa mfano ‘mama mboga’, mashuleni, migahawa midogo midogo na sehemu za vyakula.
Haya yana muundo rasmi mahsusi kuwafaa wakulima wenye mawazo ya kibiashara mpaka kwa wanunuzi wa kibiashara haswa kwa mkataba.
Wakulima wadogo wadogo wanaweza kujiunga katika upatikanaji wa kipato cha kudumu, taarifa za masoko na huduma za uwezeshwaji. Masoko kama hayo ni pamoja na wa mkataba wa kilimo kwaajili ya usafirishaji nje, wakusanyaji, maduka makubwa, maduka ya mazao ya shamba, hoteli, wasindikaji na kadhalika.
Madalali na wakusanyaji wanafanya kukumika katika kukusanya kutoka masoko yasiyo rasmi .Wanakua wanajua soko linahitaji nini na wako makini katika kiwango.
Aina zingine za masoko rasmi zinajumuisha hifadhi madhubuti za serikali kama vile Bodi ya Taifa ya Nafaka na Uzalishaji, Misaada ya chakula/ wanunuzi wa chakula cha msaada kama vile Mpango wa Chakula Duniani, Msalaba Mwekundu na kadhalika. Masoko rasmi yanahitaji wakulima kuendana na viwango madhubuti vya ubora, mahitaji sawa ya ujazo wa hakika unaofikishwa na bei ya kupanda nakushuka.
Utangazaji
Mwishoni, kama hakuna mtu anaejua kuhusu bidhaa yako: hauwezi kutarajia kuuza chochote.
Unahitaji kufikiria kuhusu namna utakayoenda kuwajulisha watu kuhusu faida za bidhaa zako au huduma.
Njia moja wapo ya kuibua ufahamu kuhusu bidhaa yako ni utumiaji wa mitandao ya kijamii kufanya matangazo. Haitakugharibu sana au chochote kabisa.
Huduma za mitandaoni kama OLX Kenya, Mkulima Young, Farm Soko na SokoPepe ni majukwaa mazuri kutangaza bidhaa yako.
Unaweza pia kuongea na madalali na kutembelea wanunuzi wa kubahatisha/ uliowagundua.
Baadhi ya wakulima pia hutegemea maongezi. Hii ni wakati watu wanawaambia wengine kuhusu bidhaa au huduma yako.Hii ni njia nzuri kwasababu watu huamini taarifa wanayopata kutoka kwa marafiki.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Fedha
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure