Kujenga banda la kuku

Chicken house

Banda zuri la kuku litawaweka kuku wako salama na wenye afya. Safisha kila siku. Funga banda kuzuia watu na wanyama kuingia ndani. Wanaweza kueneza magonjwa.

  • Jenga banda lako kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii inazuia jua kali na upepo mkali.
  • Kuta za urefu wa futi 4 kwenda juu na futi 3 wavu. Wavu unaruhusu uingiaji mzuri wa hewa.
  • Weka mapazia kwenye madirisha kuzuia upepo. Yafunge wakati wa usiku.
  • Mahali pa kuoshea miguu na viuatilifu kutazuia wadudu na magongwa. Daima vaa koti na safisha mikono wakati unahudumia kuku.
  • Tengeneza sakafu tambarare ya saruji. Sakafu za saruji ni rahisi kusafisha. Maranda ya mbao kwenye sakafu yatanyonya kinyesi yanayodondoka.
  • Kila kuku wa nyama anahitaji angalau nafasi ya futi 1 ya mraba. Hakikisha unajua kuku wangapi unapanga kufuga kabla ya kujenga banda.