Kujenga Kiota

Chicken brooder

Nunua vifaranga vya siku moja kutoka Kenchic. Tayarisha kiota kiwe tayari masaa 24 kabla ya vifaranga vyako kufika. Kiota kiwe na mwanga wa kuyosha. Kiota cha duara kitazuia vifaranga wasibanwe kwenye kona. Panua kadri vifaranga vyako vinakua.

  • Unahitaji treya 5 za kulishia na vinyueo 10 vya maji kwa kuku 500.
  • Tibu vyombo vyotte kabla ya kuvitumia.
  • Kuku yoyote asitembee zaidi ya mita 1.5 kutafuta chakula ama maji.
  • Weka jiko futi 1 juu katikati ya banda. Litawapa joto vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi 14 – 21 za mwanzo. Washa jiko masaa 6 kabla ya vifaranga kufika.
Hakikisha kuku hawapati baridi sana au joto.

Jikos in a brooding pen