Ng’ombe wa Maziwa

Kuna njia nyingi ambazo wakulima wanaweza kupata pesa kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Unaweza kutengeneza pesa kutokana na kuuza samadi, ndama wako, na muhimu kabisa uzalizaji wa maziwa mengi.

Kuwekeza kwenye ng’ombe wa maziwa kwanza unahitaji kuorodhesha gharama zote utakazokumbana nazo. Hizi ni pamoja na :

  • Banda la ng’ombe
  • Vifaa vya kukama maziwa
  • Lishe: Unaweza kupanda malisho kama Calliandra na Napier kwenye shamba lako.
  •  Madini ya kuongeza
  • Daktari wa mifugo na ada za madawa.

Bei ya ng’ombe mwenye kutarajia ndama itategemea na kumbukumbu ya kuzalisha na maziwa. Mara tu ng’ombe anapopata  ndama na kuanza kukama maziwa, unaanza kutengeneza pesa. Kwa mfano, kama ng’ombe wako anatoa wastani wa lita 20 kwa siku, unaweza kuuza lita moja kwa KSH 40 na kupata KSH 800 kwa siku.

Unaweza kuwekeza kwenye vyakula vya ziada/visismuzi ili kusaidia kuongeza uzalishaji wako wa maziwa na kupata faida zaidi.

Hata hivyo, kabla ya kuanza biashara yako ya maziwa, hakikisha unakuwa na mpango wa biashara. Mpango mzuri wa biashara utakuonyesha malengo unayotaka kufanikisha na namna unavyopanga kuyafikia. Kwa kuongezea utakuwezesha kujua soko lako.

Lazima pia uweke kumbukumbu nzuri za ufugaji wako, maziwa na mahesabu ya uendeshaji wa biashara yako. Hii itakuwezesha kufatilia kama unatengeneza faida ama la.