Uwekaji Kumbukumbu

Uwekaji kumbukumbu wa ng’ombe wako unasaidia kufatilia afya na uzalishaji wa ng’ombe wako.
- Utajua wakati atakua na joto. Angoja siku 45 baada ya ng’ombe wako kupata ndama, uwe unaangalia uke uliovimba na uchafu msafi.
- Epuka kurudia uzalishaji kwa kunakili mbegu gani ulitumia kwaajili ya uhamilishaji.
- Kama unauza ng’ombe wako, mnunuzi ataulizia kuona kumbukumbu zako.