Kudhibiti Wadudu

Brown Ear Tick

Nyunyiza na wape ng’ombe wako dawa ya minyoo ili wawe na afya. Kama ng’ombe wako ana minyoo na magonjwa kutokana na kupe, hatakua vyema na atakua kiwango duni sokoni. Hautapata bei nzuri. Ng’ombe mzuri pia anahitaji maziwa mengi.Wadudu wanaweza kuwa wan je au wa ndani.

Wadudu wa nje

Hawa ni pamoja na kupe, viroboto, chawa na nzi. Kogesha mara kwa mara ( kila baada ya wiki 2) au kunyunyiza na viuadudu iliyopitishwa kwa usahihi kama Grenade au Triatix kutoka Coopers inasaidia kudhibiti kupe kama Brown Ear Tick. Brown Ear Tick husababisha magonjwa kama Nagana ( ECF)

Jinsi ya kuogesha ng’ombe wako na Grenade au Triatix kutoka Coopers:

Hatua ya 1

Changanya bidhaa na maji kwenye knapsack. Fuata maelezo kwenye pakiti.lita 10 za mchanganyiko unatosha kwaajili ya ng’ombe 1 mkubwa au ndama 2 wadogo.

Spraying equipmentHatua ya 2

Mnyunyizie ng’ombe. Anza upande wa nyuma wa ng’ombe na nyunyiza kuelekea upande wa mbele wa ng’ombe. Hii ni kwasababu manyoya ya ng’ombe yanaota kutoka nyuma kuja mbele, hivyo dawa itafika kwenye ngozi kama utaanzia nyuma. 

Spraying cowHatua ya 3

Pulizia hivi mpaka ufikie upande wa mbele wa ngombe, Hakikisha mwili wote wa ngombe umepuliziwa. Usisahau, kwato, uso, na chini ya mkia.

Spraying cow 2Hatua ya 4

Puliza kila siku 7

Protective gearWadudu wa ndani

Wadudu wa nje haswa ni pamoja na minyoo-duara, minyoo-bapa, na kadhalika.

Wape ng’ombe wako dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3 kwa kutumia Nefluk au Nilzan kutoka Coopers. Usingoje ng’ombe wako apate minyoo kabla ya kutibu.

Nefluk and NilzanKiasi gani cha Nefluk au Nilzan unachompa ng’ombe wako ni kuendana na uzito wake. Usikisie uzito, tumia mkanda wa uzito. Kama utampa dawa kidogo ya minyoo, minyoo itakua sugu.

Weighing bandInapendekezwa kufanya unyweshaji wakati unampa dawa ya minyoo kuhakikisha ng’ombe anameza dozi yote ya dawa. Kumpa dawa ya minyoo kwa kutumia bunduki ya kunyweshea:

Deworming drenching gunHatua ya 1

Mzuie mnyama kwa kumuweka kati kati ya miguu yako( kwa wanyama wadogo) au kwa kuwaweka kwenye.

Hatua ya 2

Pima dawa kwenye chupa au bunduki ya kunyweshea kuendana na maelezo ya mzalishaji.

Hatua ya 3

Weka mkono mmoja kwenye pua ya mnyama, fungua mdomo kiasi cha kutosha kuweza kuingiza bunduki au chupa.

Hatua ya 4

Weka chupa pembeni mwa mdomo wa mnyama na hakikisha kwamba ulimi haujazuiliwa unapompa dawa.

Hatua ya 5

Shikilia mdomo uliofungwa kwa sekunde chache baada ya kutoa chupa ili dawa imezwe yote.

Drenching gun for deworming