Magonjwa na Chanjo

ECF symptoms

Njia nyingine ya kuzuia magonjwa ni kupitia chanjo. Hapa chini kuna orodha ya baadhi ya magonjwa ya kawaida unayopaswa kuchanja katika hatua tofauti. Hakikisha unapata Mtaalamu wa mifugo kuchanja ng’ombe wako. Usifanye mwenyewe.

Brucellosis

Umri: Miezi 3-8 kwaajili ya mitamba.

Upeaji:Mara moja katika maisha.

Maoni:  Wakati wa mlipuko kundi lote linaweza kuchanjwa.Tumia chanjo kwa umakini. Chanjo ya S19 inaweza kusababisha brucellosis kwa binadamu.

Anthrax and Blackquarter

Umri: Miaka 3

Upeaji: Kila mwaka au kukiwa na onyo dhidi ya mlipuko

Maoni: Chanjo inapatikana na ni ya ufanisi. Anthax ni hatari sana kwa binadamu na wanyama.

East Coast Fever

Umri: Mwezi 1 na zaidi

Upeaji: Chini ya masikio

Maoni: Wataalamu wa mifugo walio na vibali pekee ambao wamefunzwa kuhusu njia za maambukizi na tiba za kutoa ndio wanapaswa kutumiwa

Ugonjwa wa Kwato na Midomo

Umri: Wiki 2 na zaidi

Upeaji: Kila baada ya miezi 6 katika maeneo hatarishi

Maoni: Njia totauti zinatumika. Wasiliana na mtaalamu wako wa Mifugo kuhusu chagua la chanjo.

Rabies

Umri: Miezi 3 na zaidi

Upeaji: Ng’ombe anaweza kuchanjwa kila mwaka na lazima achanjwe kunapokua na mlipuko

Maoni: Hii ni chanjo pekee ambayo inaweza kukinga ng’ombe ambao wameshaathirika kama itafanywa ndani ya muda usiozidi wiki moja baada ya mlipuko. Toa ripoti ya tatizo haraka kwa mtaalamu wa mifugo katika eneo lako

Rift Valley Fever (RVF)

Umri: Miezi 6 na zaidi

Upeaji: Baadhi ya chanjo ni chanjo hai hivyo tumia kwa uangalifu. RVF kwa binadamu inaweza kuuwa hivyo kinga ni muhimu sana.

Lumpy Skin

Umri: Mwezi 1 na zaidi

Upeaji: Kuzuia kunapokua na mlipuko.

Maoni: Kama unatumia chanjo hai, tenga ng’ombe kutoka kwa kondoo na mbuzi, kwani chanjo hutokana na virusi vya pox vya kondoo vilivyo ambavyo vinaweza kusababisha pox kwenye kondoo na mbuzi.