Kabeji

Kabla haujaamua kupanda kabeji, unahitaji kuhakikisha kwamba udongo wako unafaa.Kujua hili,utahitaji kufanyia udongo kipimo/uchunguzi, ambacho kitakujulisha:

  •  Afya ya udongo wako
  • Mbolea kiasi gani utahitaji kuongeza
  • Mazao yatayakofanya vyema kwenye shamba lako.

Pigia CropNuts, huduma ya kupima udongo, Daktari Wa Udongo, kwenye +254 790 499190 au tuma barua pepe kwa support@cropnuts.com. Watachukua sampuli ya udongo wako kutoka shambani mwako na kukutumia majibu. Kipimo cha udongo kitaokoa pesa na kitakupa zao kubwa na bora.

Zinaota vyema kwenye hali ya baridi yenye nyizi joto 16-20℃, mvua iliyosambaa vizuri kwa 1500mm kwa mwaka na kati ya 800-200m.Hata hivyo kama upo kwenye eneo kame, unaweza kupanda kabeji kupitia umwagiliaji.

Udongo wenye maji na rotuba ya kutosha na viumbe hai na uchachu au pH wa kati ya 6-6.5, ni mzuri kwaajili ya kabeji.