Aina za Kabeji

Cabbage

Siku zote nunua mbegu zilizoidhinishwa. Mbegu zilizoidhinishwa :

 • Hukupa mavuno mengi na ya kiwango bora.
 • Hupunguza uwezekano wa mazao kutofaulu.
 • Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa.
 • Hukua kwa haraka, imara na kwa usawa.

Chagua aina yako ya kabeji kuendana na majibu ya kipimo chako cha udongo, hali ya hewa na hitaji la soko. Chini ni orodha ya aina zao ambazo unaweza kununua kutoka Royal Seed:

PRETORIA F1

 • Hukomaa ndani ya siku 75 tangu kupandikizwa
 • Kichwa kina uzito wa kilo 4-5
 • Uhakika wa mavuno:tani 60 kwa ekari
 • Majani mazuri yakufunika na hustahimili joto
 • Rangi ya kijani iliyokolea
 • Huhimili kunyauka/Fusarium Wilt

BLUE JAYS F1

Cabbage blue jays

 • Hukomaa mapema: Hukomaa ndani ya siku 55 baada ya kupandikizwa
 • Uzito wa kichwa: kilo 3
 • Uhakika wa mavuno: tani 50 kwa ekari
 • Majani mazuri yakufunika na hustahimili joto
 • Rangi ya samawati kijani
 • Huhimili kunyauka/Fursarium Wilt
 • Huhimili kiasi kuoza ama Black Rot

FABIOLA F1

 • Hukomaa ndani ya siku 75-80 baada ya kupandikizwa
 • Uzito wa kichwa: kilo 5
 • Uhakika wa mavuno:tani 60 kwa ekari
 • Kichwa chenye umbo la nusu bapa chenye majani mazuri yakufunika
 • Hustahimili joto
 • Huhimili  madoadoa au Ringspot
 • Huhimili vizuri wa Black Rot

COPENHAGEN MARKET

Copenhagen

 • Hukomaa mapema: Hukomaa siku 65 baada ya kupandikizwa
 • Uzito wa kichwa: kilo 2.5 – 3
 • Uhakika wa mavuno:tani 30-35 kwa ekari
 • Gharama  ya kulinda mazao ni nafuu
 • Rangi ya kijani iliyokolea na katikati unaong’aa