Maandalizi ya shamba

Ploughing land preparation

Mara tu mbegu zako zinapopadwa kwenye kitalu, lima shamba lako. Vunja madonge ya udongo. Changanya samadi iliyooza vyema. Lainisha udongo wa juu.

Kipimo chako cha udongo kitakujulisha mbolea gani za kuongeza kwenye udongo wako na kiasi gani.Kawaida utaambiwa kuongeza mbolea ya NPK wakati wa kupanda.Hii ina Naitrojeni, Fosferi na Potasiamu, na mara nyingine virutubisho vingine pia.

Mavuno Fertilizers (ARM Cement) wanatengeneza mbolea maalum kwaajili ya mazao yako. Nunua mbolea za Mavuno kutoka kwa wauza pembejeo.