Kuandaa Kitalu

Nursery

Hatua ya 1

Safisha majani na magugu/kwekwe.Chimba udongo vizuri ili kusiwe na madonge na ardhi isawazishwe.

Hatua ya 2

Wiki moja kabla ya kupanda, ongeza safu ya mbolea ya samadi iliyooza vyema ya sentimita 7.Tumia wheelbarrow 1 uliojaa mbolea ya samadi kwa kila mita 3  maraba. Changanya kwenye udongo.Mwagilia kitalu.

Hatua ya 3

Inua tuta sentimita 15-20 juu na mita 1 kiupana kisha sawazisha

Hatua ya 4

Fanya vishimo vya sentimita 3 kwenda chini na sentimita 20 kiumbali, kutumia mkono.

Hatua ya 5

Loweka mbegu kwenye mchanganyiko wa gramu 50 PEARL ndani ya lita 20 za maji kabla tu kuzipanda.Hii itasaidia kukinga magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche.

Hatua ya 6

Changanya mbegu na udongo kiasi kasha tandaza kwenye vishimo. Mwagilia maji kwa makini kisha funika mbegu taratibu na udongo kisha weka majani makavu-mulch.

Kuchipuka

Mbegu zako zitaanza kuchipuka baada ya siku 5-7. Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu

Spinach germinationKivuli kiwe mita 1 juu. Weka nyasi kwa juu lakini hakikisha jua kiasi linweza kupenya.

  • Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye tuta jingine.
  • Weka udongo kuwa na unyevu nyevu lakini usitote. Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.

Maji mengi sana

  • Virutubisho kwenye udongo huoshwa.
  • Kutakua na upungufu wa hewa safi kwenye udongo.
  • Mmea utaanguka na shina litaoza. Mmea unaweza kufa.

Maji kidogo sana

  • Mmea hufifia.
  • Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vizuri hivyo ukuaji duni.