Wadudu na Magonjwa ya Kabeji

Cutworms

Wadudu

Viwavi weusi aina ya Cutworms

Hawa ni viwavi weusi wanapatikana kawaida katika hatua za mwanzo za ukuaji wa mmea. Hukata mashina usawa wa ardhi kusababusha mmea kuanguka. Nyunyizia mmea kwa UMEME baada ya kupandikiza kudhibiti cutworms.

Kidukari

Kidukari ni mdudu mdogo wa kijani au njano anaepatikana kwenye majani ya mboga mboga. Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea na pia wanabeba magonjwa.

Nzi weupe

Hawa ni wadudu wadogo weupe wanaopatikana chini ya jani.Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea

Whiteflies cabbageSawflies na Black diamond moths

Ni kipepeo weusi wa kufifia – kijani kwa rangi na hatua yake ya buu au kiluilui ni mharibifu sana.

Wanakula majani kusababisha kupukutika. Kama hawajadhibitiwa, wanasababisha hasara ya 100% ya mazao. Nyunyizia kwa CYCLONE unapoona dalili ya kwanza ya kushambulia.

Magonjwa

Black rot

Ni bacteria kwenye udongo ambaye anaweza kusababisha hasara kabisa ya mazao kama hautadhibitiwa. Ni kawaida wakati joto ni jingi na udongo una unyevu. Dalili ni pamoja na ncha makavu ya njano au kahawia mikavu katika hatua za mwanzo za kushambulia. Baadaye, vichwa hegeuka vyeusi,laini na huanza kuoza na kutoa harusu mbaya. Kumudu, toa na haribu mabaki ya mazao yaliathirika, tumia miche misafi na yenye afya na aina inayohimili. Nyunyizia Sulcop DF kutoka Osho Chemicals, mapema na kisha rudia kila siku 10.

Madoa au Leaf Spot

Leafspot cabbageMadoa Pia ni kuvu atokanaye na udongo ambao ni kawaida kwenye hali unyevunyevu Husambazwa na  kupepo,maji au vifaa vilivyoathirika. Dalili ni pamoja na madoa ya kahawia na mwisho kufanya mashimo na majani hukauka.Kudhibiti,panda mbegu zilizoidhinishwa na badili mazao. Nyunyiza Sulcop, Control 70DF au Enrich kutoka Osho Chemicals.

Kuvu wa duara (Ringspot)

RingspotNi kuvu anaebebwa na upepo,mbolea ya samadi au mabaki ya mazao yaliyoathika.dalili ni duara- kama doa la kahawia kijivu kwenye majani.Kudhibiti,panda mbegu zilizoidhinishwa/miche yenye afya,badili mazao kwenye shamba lako.Nyuniza Sulcop au Enrich kutoka Osho Chemicals.