Utamwagilia vipi mazao yako?

Drip irrigation

Maji ya kutosha ni muhimu kwaajili ya ukuaji wa afya na uzao. Wakati mbogamboga hazina maji ya kutosha huacha kukua na mara nyingi huanza kuzalisha mbegu kabla ya kukomaa(bolting) – au kufa tu.

Kwa afya, ukuaji imara na mazao kwa wingi, kabeji zako zitaitaji maji ya kutosha kila wakati kwa mizizi yake. Lengo ni kuweka udongo au mboji katika usawa na unyevu nyevu

Umwagiliaji wa tone kwa tone (Drip)

Umwagiliaji wa tone kwa tone -drip unaweza kukusaidia kutumia maji kwa ufasaha. Mfumo wa umwagiliaji wa tone kwa tone:

  • Hutumia maji kidogo kwani maji kutoka kwenye mifereji yanaenda moja kwa moja kwenye mizizi ya mmea. Maji hayapotezwi kwenye magugu/kwekwe.
  • Mimea haitoti.
  • Mara tu mifereji ya drip inapowekwa, unatakiwa tu kufungua mfereji wakati inataka kumwagilia.

Kupata mfumo wa umwagiliaji wa tone kwa tone-drip, wapigie SunCulture kwenye +254(0)700 327 002. Unaweza pia kutembelea tovuti yao kupata nukuu ya bei.

Wakulima wa DLTP waliamua kununua pampu ya sola ya Futurepump kwa pamoja. Hii pampu inafanya kazi kwa kutumia nguvu kutoka kwenye jua.

Futurepump solar pumpUnaweza kulipia gharama za Futurepump baada ya misimu 3. Baada ya hapa, pampu yako haitaku gharimu!