Nyanya

Nyanya ni zao la kawaida sana linalolimwa na wakulima wadogo wadogo na wakubwa ndani ya Kenya.

Ni zao la msimu mfupi lenye thamani kubwa ambalo huchukua miezi 2-3 kupevuka.

Asilia, zao hili lilikua likipandwa katika maeneo ya wazi lakini muda unavyoenda, wakulima wamevutiwa na uzalishaji wa vivungulio.

Nyanya zina vitamin vingi. Kwa kawaida hutumika kama kachumbari, kama mboga inayotengenezwa kuwa sosi, mchuzi na rosti zito.

Nyanya zinafanya vyema katika hali zifuatazo:

  • Mvua ya wastani kati ya 760 – 1300mm japo inaweza kufanyika kwa umwagiliaji.
  • Joto la wastani la nyuzi joto 20 – 25 wakati wa mchana na nyuzi joto 15- 17 wakati wa usiku.
  • Mchanga mweusi –wenye rutba uliotota vyema wenye Uchachu au pH 5-7.