Usimamizi

Tomato stalking

Hatua 1: Nafasi

Wiki 2 baada ya kupandikiza,panda miche mipya ili kuchukuwa nafasi ya miche ambayo haikuota

Hatua 2: Utoaji kwekwe/nyasi

Palilia kila wiki 3-4 kuzuia wadudu, magonjwa na kuzuia ushindani kwa ajili ya virutubisho.

Hatua 3: Kujazia

Baada ya wiki 3, jazia na mbolea yenye nitrogen kama Mevuno Topdressing NPK 20.0.0. Katika wiki ya 5 kabla ya kutoa maua, ongezea tena na NPK 17:17:17 au 20:20:20. Unahitaji kilo 20/Ha.

Hatua 4: Kuweka miti

Funga mashina ya nyanya kwenye kamba kuimarisha mashina yasiyo imara. Hii inahakikisha unapata matunda safi na yasiyo na magonjwa na kufanya uvunaji kuwa rahisi.Tomato stalking 2

Hatua 5: Kupogoa

Toa mashina yanayo chipuka pembeni kubaki na mashina yenye afya pekee.

Tomato pruningHatua 6: Malisho ya majani

Weka mbolea ya majani kwa uendanaji wa virutubisho sahihi vinavyohitajika na mmea wa nyanya katika hatua tofauti za ukuaji. Kwa mfano, nyunyizia EASY GRO flower and fruit NPK 14: 11:33 wakati wa kutoa maua kuboresha utoaji wa maua na kupunguza uharibikaji wa maua.