Wadudu na Magonjwa ya Nyanya

Blossom End Rot

Wadudu

Kila mara kagua kuchunguza wadudu. Wadudu wa kawaida wanaoshambulia mimea yako ya nyanya ni pamoja na:

Nziweupe

Ni wadudu wadogo weupe ambao hujificha chini ya majani. Wananyonya na kueneza magonjwa ya virusi katika mmea wako wa nyanya. Unaweza kutumia mitego yenye mnato au gamu kutoka Real IPM( +254 725 806086), Mtayarisho wa mwarubaini kama Nimbecidine au nyunyizia na viuadudu kama ASATAF.

Whiteflies on tomatoesWatoboa matawi (Leafminers)

Mdudu hatari sana anaekula majani, shina na matunda na kunyonya majimaji. Pia wanataga mayai kwenye majani ambayo hutotolea viwavi na kula majani. Utaona mistari mieupe kwenye majani. Matunda yataoza na shamba kukauka na kuonekana kama limechomeka na moto. Kukinga, tumia njia za kibailojia kama vile Diglyphus ambayo hula leafminer.

Leafminers on tomatoesWadudu wengine

  • Vidakuri (Aphids):Utaona alama vyeupe juu ya majani.
  • Siafi baibui wekundu: Ni wadudu wadogo ambao kufanya alama vyeupe- njano kwenye majani.
  • Minyoo wa American Bull Worms na parare: Ni wadudu wanaotoboa majani.
Kukinga wadudu, palilia mapema, tumia mbegu zilizoidhinishwa na nyunyizia kwa viuadudu sahihi.

Matatizo

Muozo wa ncha( Blossom end rot)

Hili ni tatizo la kawaida linalosababishwa na upungufu wa kalsiamu au kiwango kidogo cha Uchachu au pH katika udongo. Sehemu ya chini ya tunda hupata alama nyeusi na kuanza kuoza. Kudhibiti hili fanya kipimo cha udongo kujua afya ya udongo wako na Uchachu( pH ) kila miaka 2 -3.

Nyunyiza mbolea maji au foliar Spray iliyo na kalsiamu kama Easy Gro Calcium.

Blossom End RotMagonjwa

Magonjwa mengi yanayovamia nyanya yanasababishwa na kuvu na bacteria. Haya ni pamoja na:

Kuchomeka kimapema na baadaye (Early and Late Blight)

Husababishwa na bacteria na kawaida katika msimu wa mvua. Majani na matunda yanaanza kutoa madoa meusi na kuanza kuoza. Kukinga: tumia mbegu zilizoidhinishwa/aina zinazohimili, fanya ubadilishaji wa mazao na zuia kwa viuatilifu kama Ridomil au Mistress kutoka Osho Chemicals.

Early and Late blightUkungu wa poda poda

Hufanya ukungu mweupe kwenye majani ambao hubadilisha majani kuwa njano na kukauka. Kuzuia, ondoa na angamiza mimea iliyoharibiwa na nyunyizia na viuatilifu kama Control 70DF

Kunyauka (Bacteria wilt)

Kunyauka haina tiba. Majani yatapukutika na yanaweza kukauka. Muda wote tumia aina zinazohimili, fanya ubadilishaji wa mazao na tibu udongo kabla ya kupanda. Ondoa mimea iliyoathiriwa.

Bacterial wilt tomatoesKunyauka ( Fusarium wilt)

Ni kuvu ya kawaida pia katika nyanya. Inapatikana kwenye udongo na kawaida katika msimu wa joto jingi. Dalili ni pamoja na kuwa njano na kunyauka kwa majani ya sehemu ya chini na kisha mmea wote kufa. Kukinga, panda aina zinazohimili na tibu udongo vyema kabla ya kupanda.

Kwa mengi kuhusu wadudu na magonjwa jiunge na iShamba au tuma SMS kwa 21606