Uhudumiaji wa mmea
Kwaajili ya mavuno mazuri ya Hoho, unataka utoaji sawasawa wa matunda kwenye mmea.
Virutubisho vingi vinatoka kwenye udongo. Kama kuna matunda mengi sehemu ya chini, yatatumia virutubisho vyote. Virutubisho havitasafiri kufikia matunda ya juu na yatakufa.
Kagua unyevu wa udongo
Tumia mikono yako kukagua udongo umetoete kwa kiasi gani kila siku. Kama udongo ni mkavu, mmea haiwezi kupata maji na virutubisho. Utapata mavuno mabaya. Usimwagilie maji mimea yako wakati wa jioni. Udongo utatota sana usiku kucha na utapata magonjwa zaidi.
Kutegemeza hoho zako
Matunda ya hoho ni mazito. Tegemeza/usitiri mmea wako wa Hoho kwa waya.
Funga mmea kwenye waya kwa kutumia uzi. Zungusha mmea kuzunguka uzi. Kua
mwangalifu usiumize mmea. Kutegemeza Hoho zako kunasidia mzunguko wa hewa. Utakua na wadudu
wachache na magonjwa.
Pogoa mmea wako wa Hoho kila wiki
Kupogoa kunaruhusu mmea wako kutumia maji na virutubisho kutengeneza matunda makubwa, yote yakiwa na ukubwa sawa.Toa matunda madogo na yoyote yenye umbo mbaya.
Hatua ya 1
Toa vikonyo vya pembeni. Acha vikonyo 2 kwa kila mmea. Toa majani yaliyozeeka na majani yenye magonjwa. Mmea wako utakua na afya.
Hatua ya 2
Toa matunda ya mwanzo, ili mmea ukue vyema. Toa matunda ya ziada ili yele yanayoachwa yawe makubwa.
Safisha kivungulio chako mara kwa mara
Palilia kila wiki kutumia mkono.Nyasi huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mmea wako.
Kwekwe/Magugu/nyasi pia huficha wadudu na magonjwa. Kagua wadudu na magonjwa kila siku.
Unaweza pia kuzuia kwekwe
kwa kutumia nyasi kavu kufunikia.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Pilipili Hoho
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure