Spinachi

Kabla ya kuamua kupanda spinachi, unahitaji kuhakikisha kwamba udongo wako inafaa kwaajili yake.Kujua hili,utahitaji kufanyia  kipimo cha udongo, ambacho kitakujulisha:

  •  Afya ya udongo wako
  • Mbolea kiasi gani utahitaji kuongeza
  • Mazao yatayakofanya vyema kwenye shamba lako.

Wapigie huduma ya upimaji CropNut’s, Daktari Wa Udongo, kwenye +254 790 499190 au tuma barua pepe kwa support@cropnuts.com. Watachukua sampuli ya udongo wako kutoka shambani kwako ili kupima na watakutumia ripoti.Kipimo cha udongo kitaoka pesa na kitakupa mazao makubwa na bora.

Spinachi itakua vyema kwenye udongo wenye rutuba wenye maji ya kutosha, wenye viumbe hai kwa wingi na uchachu au pH ya 6-6.5. Pia inaweza kukua katika hali ya hewa tofauti tofauti, lakini bora zaidi ni maeneo yenye nyusi joto 16-20, mvua inayo sambaa vizuri ya 1500mm kwa mwaka na nyanda za kati ya mita 800 na 2200.