Kuandaa Kitalu

Nursery

Hatua ya 1

Safisha magugu/kwekwe na nyasi zote. Lima udongo vyma mpaka kusiwe na madonge.

Hatua ya 2

Wiki 1 kabla ya kupanda, ongeza safu ya sentimita 7 ya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Tumia toroli 1 uliojaa wa mbolea kwa kila mita 3 za mraba. Changanya kwenye udongo. Mwagilia (maji) tuta.

Hatua ya 3

Loweka mbegu kwenye maji baridi kwa masaa 24 kabla ya kupanda.

Hatua ya 4

Panda mbegu kwenye mistari sentimita 2 kwenda chini kwenye mishororo ya sentimita 15 kiumbali. Funika mbegu na safu nyepesi ya udongo. Ongeza nyasi kavu kama kivuli. Hii inalinda udongo na kuhifadhi unyevunyevu . Mwagilia (maji) matuta.

Uchipukaji

Mbegu zako zitaanza kuchipuza baada ya siku 5-7.Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu.

Spinach germination

  • Kivuli kinatakiwa kuwa mita 1 juu. Weka nyasi juu yake lakini hakikisha jua kiasi linaweza kupenya.
  • Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye tuta jingine.
  • Uweke udongo kuwa na unyevu unyevu. Maji mengi sana au kidongo sana ni mbaya kwa ya miche yako.

Maji mengi sana

  • Virutubisho kwenye udongo vinaondolewa.
  • Kutakua na ukosefu wa hewa safi ya kutosha kwenye udongo.
  • Mmea utaanguka na shina litaoza.Mmea unaweza kufa.

Maji kidogo sana

  • Mmea unanyauka.
  • Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vyema hivyo ukuaji duni.