Kuandaa shamba

Land preparation

Mara tu mbegu zako zikishapandwa kwenye kitalu chako, lima shamba lako. Vunja madonge ya udongo. Changanya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Lainisha udongo wa juu.

Kipimo chako cha udongo kitakuambia mbolea gani za kuongeza kwenye udongo wako na kiasi gani.Kwa kawaida utaambiwa kuongeza mbolea ya NPK wakati wa kupanda.Hii ina Naitrojeni, Fosferi na Potasiamu, na muda mwingine virutubisho vingine.

Mavuno Fertilizers (ARM Cement) wanatengeneza mbolea maalum kwa zao lako. Nunua mbolea za mavuno kutoka kwa wauza pembejeo.

Mavuno NPKMagugu

Magugu/kwekwe huchukua maji na virutubisho kutoka kwa mmea.pia huficha wadudu na magonjwa. Toa magugu unapoyaona.

Unaweza pia kutumia dawa ya magugu. Siku zote fuata maelezo na vaa nguo za kujikinga wakati unatumia dawa za magugu.