Kuvuna

Spinach plant

Kutegemea na aina ya spinachi, spinachi  itakua tayari kwa kuvuna baada ya miezi 2-3. Katika hatua hii, itakua ishatoa/imezalisha majani makubwa, safi na yaliyokomaa.

Vuna majani mara mbili kwa wiki na tumia au peleka sokoni haraka iwezekanavyo. Utaendelea kuvuna kwenye miezi 2-3 inayofuata.

Kwa vile huharibika haraka,hakikisha kuna soko la tayari kabla ya kuvuna.