Wadudu na Magonjwa

Spinach whiteflies

Wadudu

Nzi weupe au Whiteflies

Nzi weupe au Whiteflies ni wadudu wadogo weupe ambao wananyonya utomvu kutoka kwenye majani ya spinachi.

Kidukari

Spinach aphidsKidukari ni wadudu wadogo, kawaida wana mwili wa kijani laini ambao husababisha mjani ya spinachi kujikunja.

Angamiza Nziweupe au WhiteFlies na Kidukari kwa Cyclone kutoka Osho Chemicals.Changanya mililita 30 za Cyclone kwenye lita 20 za maji ndani ya bomba/knapsack. Nyunyizia/pulizia unapoona Nzi weupe Whiteflies au vidukari.

Viwazi

Viwavi hufanya mashimo kwenye majini ya spinachi. Majani yenye matundu hayapati bei mzuri sokoni

Waangamize Viwavi kwa Mida kutoka Osho Chemicals, Changanya mililita 10 ya Mida kwa maji 20lt. Puliza ama nyunyiza kwenye matawi unapoona viwavi. Mida pia huua nzi weupe.

Spinach caterpillarsMagonjwa

Madoadoa/Leaf Spot

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuvu. Utaona vidoa vidogo vyeusi kwenye majani.Vidoa hubadilika kuwa kahawia au kijivu.

Tibu Leafspot kwa Sulcop 50DF kutoka Osho Chemicals. Changanya gramu 50 za Sulcop kwenye lita 20 za maji ndani ya bomba/knapsack. Nyunyizia majani. Hufanya kazi vizuri wakati unaitumia kudhibiti Leafspot.

Spinach leaf spotUkungu wa podapoda

Ukungu wa podapoda ni kuvu nyeupe inayoota chini ya majani ambayo baadaye hufanya madoa meusi au ya kahawia kwenye sehemu ya juu ya majani. Huanza mapema sana kwenye kitalu na kuendelea kwenye hatua zote za mmea, kama haitadhibitiwa vyema.

Spinach pests and diseases

Kudhibiti, badilisha eneo lako la shamba, fanya usafi mzuri wa kitalu na tibu kutumia Control kutoka Osho Chemicals.