Aina za Spinachi

Swiss chard fordhook

Wakulima wa DLTP wamenunua aina ya Fordhook Giant kutoka Royal Seed ambayo:

  • Inaota vyema, hata kwenye hali ya hewa ya joto
  • Ina majani makubwa na
  • Inakua mpaka sentimita 65
  • Inakomaa siku 60-70 baada ya kupandikizwa.

Daima nunua mbegu zilizoidhinishwa. Asilimia 95-100 ya mbegu zitaota, hivyo utatumia mbegu kidogo. Mbegu zilizoidhinishwa:

  • Hutoa mavuno mengi na kiwango bora.
  • Huhimili baadhi ya magonjwa
  • Hukua kwa haraka, imara na usawa”

Nunua mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wauza pembejeo. Mbegu za Fordhook Giant huja kwenye ujazo wa gramu 10, gramu 25, gramu 50, gramu 100, gramu 250, gramu 500.

Aina nyingine za spinachi, ambazo hupandwa sana, ni pamoja na Lucullus, Early Hybrid No.7, Bloomsdale, Giant, King of Denmark na New Zealanda Spinach.