Viazi

Ukulima wa viazi unafaida nzuri. Wakulima wanakumbana na matatizo katika upandaji wa viazi. Kama haupandi viazi vyako vizuri, utavuna viazi vidogo na vya ubora wa chini.

Viazi mbatata (Viazi vya kuzungu) vinaota vyema katika maeneo yanayopata mvua za mara kwa mara za 900mm – 1400mm kwa mwaka, na yenye hali ya hewa tulivu pamoja na joto kati ya nyuzi joto 10 -23.

Hufanya vyema katika usiogandana, laini, wenye kutota vyema, na wenye uchachu kidogo. Udongo usiotota vizuri mara nyingi husababisha viwango duni na mazao kidogo. Udongo mzito unaweza kusababisha mashina kuwa madogo na yanayokwaruza.

Kabla ya kupanda eneo la viazi, peleleza historia ya shamba kwa mfano, kama karibuni limetumika kupanda zao la jamii yake kama Nyanya, biringanya, hoho nakadhalika. Magonjwa sawa au yale yale yanadhuru haya mazao kama vile Bacteria wilt, ambayo hayana tiba.