Uchaguaji wa mbegu

Potato seed selection

Wakulima wengi wanatumia mbegu ambazo wameweka kutoka zao la mwaka jana na ambazo wametumia kwa miaka kadhaa. Hii ina maanisha mbegu hazina nguvu na mara kwa mara huwa na magonjwa, ambayo hufanya zisiweze kukupa mavuno mazuri.

Tumia mbegu zilizoidhinishwa. Hizi ni mbegu ambazo:

  • Hukua kwa haraka
  • Hazina magonjwa.
  • Hutoa mazao mengi
  • Hupata bei nzuri sokoni
  • Utapata viazi mbegu za viazi zilizoidhinishwa kutoka kwa wasambazaji wazuri.
  • Kama ukitumia mbegu kutoka shambani kwako, chagua na weka alama zenye afya wakati zinaendelea kukua.