Kuhifadhi Viazi

Charcoal cooler

Uhifadhi wa viazi pia nguzo muhimu ya kupata mavuno mengi. Kuhifadhi viazi vyako kuna faida nyingi nzuri.

Sio tu utazuia kupoteza kiasi flani cha mavuno yako kila mwaka kwa magonjwa, pia unaweza kuyaweka mpaka muda ambapo soko ni zuri.

Unda kikundi na majirani zako ili kuwauzia wanunuzi wakubwa. Ni rahisi kuuza magunia 1000 kuliko magunia 100. Utapata faida kubwa.Hifadhi viazi vyako katika ghala la makaa

Njia nzuri ya kuhifadhi viazi vyako ni kutumia ghala linalopoozwa na mkaa

Jenga ghala kubwa la mkaa na majirani zako. Hifadhi mazao yako ya viazi mpaka miezi 3 -4.

Kuta za wazi zinatengenezwa na waya wa vyavu uliojazwa mkaa.

Mkaa muda wote huwekwa ukiwa na uvyevu kutoka kwenye tenki. Maji huwa mvuke kutoka kwenye mkaa inapo chukua joto kutoka ndani ya ghala. Hivyo ghala huwa na hali ya baridi sana. Pia lina giza – Hali mzuri sana kwaajili ya viazi!

Hakikisha magunia hayagusi kuta

potatoes in charcoal store

Faida za ghala la mkaa

  • Hakuna stima inayohitajika, ni maji tu.
  • Linaweza kutumika kuhifadhia matunda totauti na mboga mboga.
  • Huzuia matunda na mboga mboga kukauka
  • Rahisi kujenga.
  • Kama wakulima wengi wanajiunga pamoja kujenga ghala, sio ghali.
  • Rahisi kudumisha.