Malisho
Kutengeneza maziwa mengi mazuri, ng’ombe wa maziwa wanahitaji lishe bora
ya aina tofauti, ikiambatana na nguvu, mchanganyiko wa kiwango, protini,
vitamin na madini.
Nguvu
Unapolisha ng’ombe wako, mpe mchanganyiko wa chakula kikavu nusu na malisho mabichi nusu.
Malisho mabichi
Malisho mabichi hususani huwa nia mjani kama vile nyasi za Napier, Lucerne na majani ya viazi vitamu na mengineyo. Hivi huwa vina maji mengi.
- Usilishe nyasi zilizotoka tu kukatwa kwa ng’ombe wako. Kata majani mabichi na uyaache sehemu yenye giza kufifia, kisha kata kata vipande vya inchi 2 ( 5cm) ili kumrahisishia ng’ombe wako kula. Hii haitapoteza malisho.
- Ng’ombe wa maziwa anatakiwa kupewa kilo 15-20 za majani mabichi kwa siku, inapendekezwa kwa awamu mbili kwa mfano.moja asubuhi na nyingine jioni.
Malisho makavu
Malisho yanajumuisha vitu kama Mabua ya ngani, Mabua ya mpunga, Mabua ya mahindi na mazao mengine ya mboga mboga
- upande wa mabua na pia kiwango kibaya.
- Changanya sehemu moja ya malisho mabichi na sehemu moja ya malisho makavu kwa mfano gunia 1 la nyazi za Napier zilizokatwa katwa na gunia 1 la mabua ya ngano yaliyokatwa katwa.
Protini na chakula cha ziada
Dania
Dania ni chanzo kizuri cha protini. Ng’ombe wako wanatumia protini kwaajili ya kujenga mwili na kuzalisha maziwa mengi ya kiwango bora.
Kilo 5 za Dania kwa siku ni protini ya kutosha kwa ng’ombe wako. Kama ng’ombe wako hawezi kupata protini ya kutosha kutoka kwenye malisho, tumia chakula cha ziada kama Kupakula kutoka Cooper-K Brands.
Chakula cha ng’ombe wa maziwa
Chakula cha ng’ombe wa maziwa kitampa ng’ombe vitamin, nguvu na protini katika njia ya uwiano, ili ng’ombe aweze kuzalisha maziwa mazuri na kuwa na uzito wa mwili wenye afya. Unga Farm Care (EA) wanapendekeza kulisha ng’ombe wako kilo 1 ya Fugo Dairy Meal kwa kila lita 2 za maziwa ng’ombe anazokupatia zaidi ya lita 5 za kwanza.
Hivyo, kama ng’ombe wako anakupa lita 7 kwa siku: 7-5 =kilo 1 ya dairy meal.
KupaKula
Kwa ng’ombe wanaotoa lita 5 – 10 za maziwa kwa siku, wape gramu 400 za Kupakula. Mpe nusu asubuhi na nusu jioni. Kwa ng’ombe wanaotoa zaidi ya lita 10, ongeza gramu 400 kwa siku kila kwa lita 5 zaidi za maziwa juu ya lita 10. Hivyo kwaajili ya lita 20 , mpe kilo 1.2 kwa siku.
Vitamini na Madini
Kumpa ng’ombe wako madini kutafanya biashara yako ya ng’ombe wa maziwa kuwa nzuri. Ng’ombe wako atapata joto siku 60 baada ya kupata ndama hivyo utapata ndama ndani ya mwaka. Madini pia ni mazuri kwaajili ya uzalishaji wa maziwa na hali ya mwili. Madini ya poda, kama Maclik Plus na Maclik Super kutoka Cooper- K Brands ni mazuri kwaajili ya ng’ombe wakubwa. Changanya madini na chakula.
Maclik Plus
Kwaajili ya mtamba na ng’ombe aliekausha mwenye mimbaMpe gramu 10 ( ½ glasi) ya Maclik Plus kila siku.
Maclik Super
Kwaajili ya ng’ombe anaekamuliwa
Mpe gramu 200( glasi 1 ) ya Maclik Super kila siku.
Panda malisho mazao yako ya malisho kama Dania na Nyasi za Napier. Tumia samadi kutoka kwa ng’ombe wako kama mbolea.
Maji mengi
Maziwa yanatumia maji mengi. Unahitaji kuwapa ng’ombe wako maji safi mengi kila siku. Toa maji kwenye chombo cha maji kila baada ya siku 3 na weka maji safi. Hii inazuia magonjwa.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Ng’ombe wa Maziwa
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure