Uzalishaji ng’ombe

Cow with swollen vulva

Uhamilishaji (AI) ni njia bora ya kuboresha ng’ombe wako. Chagua mbegu kwaajili ya ng’ombe wako kutokana na utakavyomtumia ndama.

Kama unataka maziwa mengi utahitaji kuzalisha kwaajili ya:

  • Kiwele kizuri( imara, mraba na chuchu zenye nafasi vyema)
  • Miguu mizuri ( iliyonyooka, mipana na imara)
  • Uzalishaji mzuri( huzalisha kiurahisi, kuzaa kirahisi)

Mbegu za CRV kutoka Coopers ni nzuri sana na kuna machaguo mengi. Vhagua mbegu kabla ng’ombe wako hajapata joto, ili uwe na uhakika unapata mbegu unayotaka. Usiache mtaalamu wa mifugo akuchagulie.

Cow on heat signs

CRV catalogueMpigie simu mtaalamu wako wa mifugo mara tu unapoona dalili za ng’ombe kuwa na joto. Ng’ombe wako lazima ahudumiwe masaa 12-18 baada ya kuona uke uliovimba na ute msafi. Unapoona damu, umeshachelewa. Ng’ombe wako alikua kwenye joto siku 3 zilizopita. Itabidi ungoje mpaka siku 18-22 zijazo za joto kabla ya kufanya uhamilishaji.

 

Angalizo: Kama uchafu ni mweupe, njano au una harufu, mpigie simu mtaalamu wako. Ng’ombe wako anaweza kuwa na maabukizi.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea wavuti wa CRV kwenye www.crv4all.com au wakala wa Coopers aliye karibu nawe. Unaweza kuwapigia Coopers kwenye Simu: +254 20 420 6000.