Aina za Kabeji
Siku zote nunua mbegu zilizoidhinishwa. Mbegu zilizoidhinishwa :
- Hukupa mavuno mengi na ya kiwango bora.
- Hupunguza uwezekano wa mazao kutofaulu.
- Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa.
- Hukua kwa haraka, imara na kwa usawa.
Chagua aina yako ya kabeji kuendana na majibu ya kipimo chako cha udongo, hali ya hewa na hitaji la soko. Chini ni orodha ya aina zao ambazo unaweza kununua kutoka Royal Seed:
PRETORIA F1
- Hukomaa ndani ya siku 75 tangu kupandikizwa
- Kichwa kina uzito wa kilo 4-5
- Uhakika wa mavuno:tani 60 kwa ekari
- Majani mazuri yakufunika na hustahimili joto
- Rangi ya kijani iliyokolea
- Huhimili kunyauka/Fusarium Wilt
BLUE JAYS F1
- Hukomaa mapema: Hukomaa ndani ya siku 55 baada ya kupandikizwa
- Uzito wa kichwa: kilo 3
- Uhakika wa mavuno: tani 50 kwa ekari
- Majani mazuri yakufunika na hustahimili joto
- Rangi ya samawati kijani
- Huhimili kunyauka/Fursarium Wilt
- Huhimili kiasi kuoza ama Black Rot
FABIOLA F1
- Hukomaa ndani ya siku 75-80 baada ya kupandikizwa
- Uzito wa kichwa: kilo 5
- Uhakika wa mavuno:tani 60 kwa ekari
- Kichwa chenye umbo la nusu bapa chenye majani mazuri yakufunika
- Hustahimili joto
- Huhimili madoadoa au Ringspot
- Huhimili vizuri wa Black Rot
COPENHAGEN MARKET
- Hukomaa
mapema: Hukomaa siku 65 baada ya kupandikizwa
- Uzito wa kichwa: kilo 2.5 – 3
- Uhakika wa mavuno:tani 30-35 kwa ekari
- Gharama ya kulinda mazao ni nafuu
- Rangi ya kijani iliyokolea na katikati unaong’aa
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Kabeji
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure