Kuandaa Kitalu
Hatua ya 1
Safisha majani na magugu/kwekwe.Chimba udongo vizuri ili kusiwe na madonge na ardhi isawazishwe.
Hatua ya 2
Wiki moja kabla ya kupanda, ongeza safu ya mbolea ya samadi iliyooza vyema ya sentimita 7.Tumia wheelbarrow 1 uliojaa mbolea ya samadi kwa kila mita 3 maraba. Changanya kwenye udongo.Mwagilia kitalu.
Hatua ya 3
Inua tuta sentimita 15-20 juu na mita 1 kiupana kisha sawazisha
Hatua ya 4
Fanya vishimo vya sentimita 3 kwenda chini na sentimita 20 kiumbali, kutumia mkono.
Hatua ya 5
Loweka mbegu kwenye mchanganyiko wa gramu 50 PEARL ndani ya lita 20 za maji kabla tu kuzipanda.Hii itasaidia kukinga magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche.
Hatua ya 6
Changanya mbegu na udongo kiasi kasha tandaza kwenye vishimo. Mwagilia maji kwa makini kisha funika mbegu taratibu na udongo kisha weka majani makavu-mulch.
Kuchipuka
Mbegu zako zitaanza kuchipuka baada ya siku 5-7. Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu
Kivuli kiwe mita 1 juu. Weka nyasi kwa juu lakini hakikisha jua kiasi linweza kupenya.
- Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye tuta jingine.
- Weka udongo kuwa na unyevu nyevu lakini usitote. Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.
Maji mengi sana
- Virutubisho kwenye udongo huoshwa.
- Kutakua na upungufu wa hewa safi kwenye udongo.
- Mmea utaanguka na shina litaoza. Mmea unaweza kufa.
Maji kidogo sana
- Mmea hufifia.
- Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vizuri hivyo ukuaji duni.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Kabeji
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure