Kupandikiza miche yako

Transplanting cabbage

Pandikiza miche baada ya wiki 3-4. Pandikiza asubuhi mapema (saa 12-4 asubuhi) au jioni sana ( saa 10-12 alasiri). 

Siku moja kabla ya kupandikiza,ondoa kivuli kwenye kitalu na punguza umwagiliaji. Hii inaitwa mgandisho/imarisho. Unaipa miche nafasi ya kuzoea jua kali.

Hatua ya 1

Chimba mashimo ya kupandia kama ifuatavyo futi 2(sentimita 60) kwa futi 2 ( sentimita 60) kwaajili ya kabeji.

Cabbage transplantingHatua ya 2

Weka gramu 5( kifuniko cha chupa) cha mbolea ya kupandia kama MAVUNO VEGETABLES NPK 20:10:18 au MAVUNO PLANTING NPK 10:26:10 kwenye kila shimo. Unahitaji kilo 50 kwa kila ekari.

Hatua ya 3

Ongeza ujazo wa kiganja wa mbolea ya samadi iliyooza vyema na changanya mbolea, samadi na udongo vizuri.

Hatua ya 4

Weka mche kwenye kila shimo na imarisha shina.

Cabbage plantingHatua ya 5

Mwagilia maji vyema.

Hatua ya 6

Loweka  udongo kwa mchanganyiko wa mililita 10 za MIDA & mililita 20 za PEARL ndani ya lita 20 za maji. Hii itasaidia kuzuia wadudu na magonjwa ya mapema.

Dhibiti magugu/kwekwe

Palilia shamba lako wiki 2-3 baada ya kupandikiza. Palilia kwa umakini kutumia jembe ili kuepuka kuharibu mizizi. Magugu hung’ang’ania virutubisho na mimea yako na pia huficha wadudu wanaobeba magonjwa

Kujazia

Baada ya kupalilia, jazia na mbolea ya Niatrojeni. Hii itahamasisha uundwaji wa majani zaidi. Weka mbolea kama MAVUNO Topdressing NPK 26:0:0 au CAN. Unahitaji kilo 50 kwa ekari.

Mbolea au Vyakula vya majani

Kutokana na kile kinachokosekana kwenye udongo wako na uhitaji wa mazao tofauti, unaweza kuhitaji kulisha majani mbolea majimaji kwaajili ya vuno kubwa. Aina ya lishe ya jani ya kutumia inategemea na hatua iliyofikia mmea wako na nini mmea unahitaji.Kwa mfano:

  • Easy Starter (N.P.K 18:20:21 + T.E) Lishe jani yenye uwiano mzuri na iliyo na fesferi  na potasiamu nyingi huwezesha miche kustawisha mizizi imara.
  • Easygro Vegetative (N.P.K 27:10:16 + T.E): Mbolea yenye Naitrojeni nyingi inapendekezwa wakati wa kutengeneza mboga/jani.Nyunyizia kila vuno kwa nafasi ya wiki 2.